Mabadiliko ya kufurahisha kwenye Uwanda wa Juu wa Huangtu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 15, 2021

(Picha zinatoka tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

Septemba 13, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama Xi Jinping alifanya ukaguzi huko Yulin mkoani Shanxi, ambapo alifahamishwa kuhusu kazi ya kudhibiti mmomonyoko wa ardhi na ujenzi wa ustaarabu wa mazingira ya asili.

Sura ya mtelemko wa juu wa udongo wa manjano huko imebadilika sasa, ambapo popote pale pamefunikwa kwa miti inayostawi. Mabadiliko hayo makubwa yalitokana na utekelezaji wa mradi wa kurudisha eneo la misitu na malisho lililotumiwa kwa kilimo, na kupatanisha uhusiano kati ya binadamu na mazingira ya asili.

Mwezi Januari, 1969, Xi Jinping aliyekuwa na umri chini ya miaka 16 alifika Kijiji cha Liangjiahe cha Wilaya ya Yanchuan mjini Yan'an kufanya kazi pamoja na wakulima, baadaye alichaguliwa kuwa katibu wa kamati ya Chama ya eneo la vijiji la huko, akawaongoza wakulima katika kujenga barabara na maboma, na kuboresha hali ya uzalishaji wa mazao.

(Picha zinatoka tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

Mkoa wa Shanxi ulikuwa moja kati ya mikoa yenye hali mbaya zaidi ya mmomonyoko wa ardhi nchini China. Mwaka 1999, Kamati Kuu ya Chama na Baraza la Serikali la China viliamua kufanya majaribio ya ujenzi wa mradi wa kurudisha eneo la misitu na malisho lililotumiwa kwa kilimo katika mikoa mitatu ya Sichua, Shanxi na Gansu. Kwa kufuata utekelezaji wa sera husika mbalimbali, hasa utekelezaji wa hatua madhubuti wa sera ya kujenga ustaarabu wa mazingira ya asili tangu Mkutano Mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China ulipofanyika, uwanda wa juu wa udongo wa manjano mkoani Shanxi umebadilisha sura yake, popote pale kuna miti inayostawi, miti hiyo ya aina mbalimbali si kama tu imelinda mazingira ya asili, bali pia imekuwa chanzo cha kuongeza mapato kwa wakulima wa huko.

Hivi sasa hali motomoto ya ustawi imeonekana kwenye uwanda wa juu wa udongo wa manjano...  

(Picha zinatoka tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha

亚洲熟妇专区图