Mkutano mkuu wa 76 wa Umoja wa Mataifa wafunguliwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 15, 2021

Tarehe 14, mkutano mkuu wa 76 wa Umoja wa Mataifa ulifunguliwa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York.

Mwenyekiti wa mkutano mkuu wa 76 wa Umoja wa Mataifa, Bw. Abdullah Shahid alipotoa hotuba alitoa wito wa kutaka dunia ikumbatie “matumaini”, na akifanya majumuisho kuhusu kazi yake muhimu ya siku za mbele kuwa “nuru tano za matumaini” : kujitoa kutoka kwenye janga la Corona, kuhimiza ufufukaji endelevu, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na matatizo mengine ya mazingira, kuheshimu haki za watu wote, na kuujenga upya Umoja wa Mataifa.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Guterres alisema kwamba, anatumai nchi zote ziharakishe hatua za kukabiliana na maambukizi ya Corona, kujikita katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, na kukomesha vita. Alitoa wito wa kushikilia tena mtazamo wa awali wa Umoja wa Mataifa kuhusu thamani ya mambo: kulinda haki za binadamu, kuwahurumia wanyonge, kupata amani kwa kupitia mazungumzo, na kushirikiana na kusaidiana katika kukabiliana na changamoto za pamoja.

(Wahariri wa tovuti:Li Yidan,Zhao Jian)

Picha

亚洲熟妇专区图