Ushirikiano kati ya China na Afrika kwenye sekta ya anga ya juu wahimizwa kwa kufuata hali halisi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 24, 2021

Katika miaka hii ya karibuni, ushirikiano wa sekta ya anga ya juu umekuwa sekta muhimu na sehemu inayong’ara ya hatua ya ushirikiano katika kuhimiza ushirikiano kati ya China na Afrika, na mafanikio makubwa yamepatikana katika ushirikiano wa aina mbalimbali katika kuagiza na kuuza satelaiti, kujenga pamoja miundo mbinu kwenye anga ya juu, kunufaika pamoja na raslimali za satelaiti, na kufanya utafiti na kuendeleza satelaiti. Teknolojia ya kisasa kuhusu anga ya juu imeonesha umuhimu mkubwa zaidi katika kusukuma mbele maendeleo ya jamii na uchumi ya nchi za Afrika, na kuleta manufaa kwa maisha na uzalishaji wa watu wa Afrika.

Ripoti iliyotolewa na shirika la sekta ya anga ya juu la Afrika “Mamlaka ya Anga ya Juu ya Afrika” ilionesha kwamba, mwaka jana bajeti iliyotumika kwenye kuendesha miradi ya anga ya juu ya nchi za Afrika imekuwa mara mbili kuliko zamani. Inatazamiwa katika miaka mitatu ijayo, satelaiti zitakazorushwa na nchi za Afrika zitaongezeka na kufikia 110. Ofisa wa Mamlaka ya anga ya juu ya Umoja wa Afrika alisema kwamba, China ni mshirika na rafiki muhimu wa Afrika katika kutimiza ndoto kuhusu anga ya juu. Katika miaka hii ya karibuni, ushirikiano kati ya China na Afrika katika sekta ya anga ya juu unaendelea kupanuka kwenye kazi ya kufanya utafiti, kuendeleza na kutengeneza satelaiti, hii inahimiza uwezo wa nchi za Afrika wa kujiendeleza katika mambo ya anga ya juu.

(Wahariri wa tovuti:Li Yidan,Zhao Jian)

Picha

亚洲熟妇专区图